November 29, 2014



Falcao nje, Cavani ndani ya Utd
MANCHESTER United imepanga kumuachia mshambuliaji wao wa mkopo, Radamel Falcao kutokana kuwa majeruhi lakini inataka kumsajili straika wa PSG, Edinson Cavani na imemtengea pauni milioni 50.
Chanzo: Daily Express


Liverpool na Arsenal ndani ya vita
KLABU za Liverpool na Arsenal zipo kwenye vita ya kumuwania kipa wa Real Madrid, Iker Casillas ambaye kiwango chake kimeonekana kushuka huku Madrid wakitaka kumsajili kipa wa United, David De Gea.
Chanzo: Daily Express

Arsenal yajisogeza kwa Vlaar
KLABU ya Arsenal imejipanga kupeleka dau la pauni milioni 8 kwa Aston Villa ili kupata saini ya beki wa kati wa kikosi hicho, Ron Vlaar. Beki huyo pia anawaniwa na Manchester United.
Chanzo: Daily Express

Roma kupambana na Liverpool kwa Neto
KLABU za Roma na Liverpool zipo kwenye mchuano mkali wa kumuwania kipa wa Fiorentina, Neto, Mbrazili huyo anatarajiwa kumaliza mkataba wake mwishoni mwa msimu huu.
Chanzo: Daily Star

Dybala kuwakamua Arsenal
KLABU ya Arsenal inajipa matumaini ya kumsajili mshambuliaji wa klabu ya Palermo, Pablo Dybala. Mmiliki wa Palermo, Maurizio Zamparini, anaamini dau la mchezaji huyo ambaye uchezaji wake unafananishwa na Cristiano Ronaldo ni pauni milioni 31.
Chanzo: Daily Star

Inter ipo mstari wa mbele kwa Van Persie
KOCHA wa Inter Milan, Roberto Mancini anaamini kuwa Robin van Persie ndiye mchezaji wa kwanza kumsajili kwenye kikosi hicho, lakini hata hivyo anaweza kukumbana na upinzani kutoka kwa Man City.
Chanzo: The Telegraph

Ledesma ategwa England
KIUNGO wa Lazio, Cristian Ledesma anatakiwa kwa mkopo wa miezi sita na timu ya Arsenal kwenye usajili wa Januari. 
Chanzo: Daily Express
United yajisogeza kwa Kurzawa
KLABU ya Manchester United ipo mstari wa mbele kumuwania beki wa kushoto wa Monaco, Layvin Kurzawa, 22 kwenye usajili wa Januari.
Chanzo: Talk Sport

WASIFU
JINA                      Edinson Roberto Cavani Gómez
KUZALIWA          14 Februari 1987
ALIPOZALIWA     Salto, Uruguay
UREFU                    1.88 m (6 ft 2)
NAFASI                   Straika
TIMU                       Paris Saint-Germain
Namba                    9


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic