November 29, 2014


Mshambuliaji wa vinara wa Ligi Kuu Bara, Mtibwa, Mussa Hassan Mgosi, amesema anamsubiria kwa hamu uwanjani kiungo mkabaji Mbrazili, Emerson de Oliveira.

Emerson anafanya majaribio na Yanga na endapo atafuzu basi atapewa mkataba kwa ajili ya kuziba nafasi ya Mbrazili mwenzake, Geilson Santana ‘Jaja’ aliyeshindwa kurudi nchini kutokana na kukumbwa na matatizo ya kifamilia.

Mgosi amesema kuwa yeye anasubiri kuona uwezo wake uwanjani na siyo maneno yanayozungumzwa kwani hata Jaja alipokuja kulikuwa na maneno mengi sana lakini kiwango chake kilikuwa cha kawaida kuliko hata wachezaji wa Kibongo.


“Emerson ni mchezaji wa kawaida na hata anaweza kupitwa na wachezaji wa Kibongo, hivyo kuja kwake sioni kama kuna kigeni na tunamsubiri kwa hamu kubwa uwanjani ili tuone yaliyomo yamo,” alisema Mgosi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic