Inawezekana mechi
ya kirafiki kati ya Argentina dhidi ya Ureno ikakosa watu wengi.
Mechi hiyo
inapigwa kwenye Uwanja wa Old Trafford mjini Manchester, leo saa 4:45 usiku.
Hadi mchana
tiketi 36,000 ambazo ni nusu ya uwanja huo ndiyo zilikuwa zimekatwa.
Hali hiyo
imeonyesha kuwapa hofu waandaaji kwamba huenda kukawa na watazamaji nusu
uwanja.
Awali
ilionekana wengi wangegombea tiketi kutokana na ujio wa Lionel Messi lakini Cristiano
Ronaldo alikuwa anarejea tena OT.
Bei ya tiketi
ilikuwa pauni 40 hadi 60 kwa wakubwa na 20 hadi 30 kwa watoto.
0 COMMENTS:
Post a Comment