November 18, 2014


Makamu wa Rais wa Simba, Geofrey Nyange ‘Kaburu’ amesema ameshitushwa na kauli za baba mzazi wa kiungo wa Yanga, Simon Msuva.

Happygod Msuva, Baba mzazi wa Msuva alihojiwa na vyombo vya habari na kusema kuwa Simba walioeleza kumsaka mwanaye waachane naye kwa kuwa aliwahi kumpeleka Simba, Kaburu akaonyesha kutomjali.

Akizungumza na SALEHJEMBEA, Kaburu amesema ameshangazwa na kauli hiyo ya mzazi wa Msuva kwa kuwa hakumbuki kama aliwahi kuonana naye, wala aliwahi kumuona kiungo huyo Simba.

“Kweli sijawahi kuzungumza na baba Msuva, simjui, sijawahi kumuona na Msuva sikuwahi kumuona halafu nikampuuzia.
“Niseme nimesikitika, sidhani kama ni sahihi kumsingizia mtu kitu ambacho hakipo.

“Ukizungumza naye mwambie kama tumewahi kuonana au kuzungumza. Muulize kama kweli aliwahi kumleta Msuva halafu akaonana na mimi, huu si uungwana,” alisema Kaburu.
Hivi karibuni, Simba kupitia Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili, Zacharia Hans Poppe ilitangaza nia yake ya kumsajili Msuva.


Lakini baba wa Msuva, akaibuka na kusema Simba waachane na mtoto wake kwa kuwa aliwahi kumpeleka, wakambeza na aliyehusika na hilo ni Kaburu.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic