November 19, 2014


Baada ya kumsajili beki kisiki na mzoefu, Azam FC inalazimika kumuacha beki mmoja kati ya watatu wa kati ilionao.

Azam FC ina mabeki imara watatu wa kati ambao ni Said Morad, David Mwantika na nahodha Aggrey Morris.

Kutokana na kumsajili Wawa, hakuna ubishi Azam FC wanalazimika kumuacha Morad ambaye Simba imeanza kumtupia ndoano.
Azam FC imekuwa ikitumia mabeki watatu wanaopokezana na hakuna shaka itaendelea kutumia mfumo huo huo kwa Wawa, Mwantika na Morris.

Simba inajua ni wakati mwafaka kwao kumuachia Morad ili waliobaki wawe na nafasi nzuri ya kucheza.

Sasa safu ya ulinzi ya Azam FC itaongozwa na Wawa na Aggrey na Mwantika atalazimika kusubiri.

Lakini kulingana na mchezo au Kocha Omog akitaka kumpumzisha mmoja, basi Mwantika pia atapata nafasi ya kucheza.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic