November 12, 2014



Na Mwandishi Wetu
Beki wa zamani wa Simba, Komambil Keita amewaita viongozi wa klabu hiyo nchini Nigeria wakafanye mazungumzo.

Keita raia wa Mali anakipiga nchini Nigeria katika klabu ya Highland FC na ametamba kuwa yuko katika kiwango cha juu kabisa.
Keita ameiambia SALEHJEMBE kutoka Nigeria kuwa amepata taarifa za Simba kuwa na matatizo katika safu ya ulinzi.
“Nimesikia tu kwa kuwa nimekuwa nikiifuatilia Simba na ligi ya Tanzania. Kama wako tayari waambie waje Nigeria.
“Kama maslahi yatakuwa mazuri, niko tayari kuja kujiunga tena na Simba maana ni timu ninayoipenda na tatizo la ulinzi litafikia mwisho,” alijigamba Keita.
Keita alikuwa mmoja wa mabeki tegemeo wa Simba wakati kikosi hicho kipo chini ya Kocha Patrick Liewig raia wa Ufaransa.

Lakini baadaye aliulaumu uongozi wa Aden Rage kumcheleweshea malipo yake, mwisho akaamua kuondoka kwenda Nigeria hasa baada ya kuwa na taarifa kwamba anataka kuachwa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic