December 18, 2014


Mshambuliaji mpya wa Yanga, Amissi Tambwe amesema amezoea haraka sana katika kikosi chake kipya.


Tayari ameanza mazoezi na Yanga na kusema amezoea haraka, huenda kwa kuwa anafahamiana na watu wengi.

“Sikupata tabu, unajua wachezaji wengi tunafahamiana. Tumekuwa tukikutana uwanjani au sehemu nyingine.

“Sikupata shida sana, kwa kweli nimefanya mazoezi vizuri na mambo yamekwenda vizuri kwa kweli,” alisema Tambwe.

Saa chache baada ya kutemwa na Simba, Tambwe alijiunga na Yanga kwa mkataba wa mwaka mmoja.

Yanga ilimwaga kitita kumsajili Mrundi huyo ambaye msimu uliopita aliibuka mfungaji bora kwa kupachika mabao 19.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic