December 18, 2014

KIONGERA AKITIBIWA HUKU AKIENDELEA KUCHATI NA SALEHJEMBE...
Mshambuliaji Paul ‘Modo’ Kiongera amesema anaendelea vizuri zaidi na ameishaanza mazoezi.

Kiongera amefanyiwa upasuaji wa goti nchini India.
Mkenya huyo amemuambia rafiki wake wa karibu kwamba alikuwa na hofu na upasuaji huo lakini sasa anajisikia vizuri.

“Ameishaanza na mazoezi, ile hofu sasa imeisha kwa kuwa anaona anapona haraka,” alisema rafiki yake huyo.


Kiongera aliumia akiichezea Simba katika mechi yake ya kwanza tu ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Coastal Union.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic