December 11, 2014

UZI WA UGENINI...
Kampuni maarufu ya kuuza matairi na betri za magari ya Bin Slum Tyres Ltd, leo imeikabidhi timu ya Ndanda FC jezi mpya pamoja na vifaa mbalimbali.

Ndanda FC inayoshiriki Ligi Kuu Bara, imepokea vifaa kutoka Bin Slum ambao ni wadhamini wake wakuu kupitia matairi yake ya Vee Rubber.
UZI WA NYUMBANI.
Makabidhiano hayo yalifanyika kwenye ofisi za Bin Slum barabara ya Lumumba jijini Dar es Salaam na Ndanda iliwakilishwa na katibu wake, Edmund Njowoka.


Kwa upande wa jezi ambazo ni za kisasa zaidi, Ndanda FC walikabidhiwa za nyumbani, pia za ugenini.

Bin Slum pia ni wadhamini wa timu nyingine mbili zinazoshiriki Ligi Kuu Bara ambazo ni Stand United ya Shinyanga (Wanaidhamini kupitia matairi ya Double Star) na Mbeya City ya Mbeya (Wanaidhamini kupitia betri za RB).

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic