December 14, 2014

BWANA ESCROW AKIENDELEA KUSHUHUDIA MECHI HIYO KWA MAJONZI MAKUBWA.
 Kijana mmoja shabiki wa Yanga, aliamua kujipandika jina la Escrow na kuibuka Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kushuhudia mechi ya kirafiki ya watani, jana.

Ushindi wa mabao 2-0 waliopata Simba, ulionyesha kumchanganya Escrow ambaye hakuwa na amani muda wote.
Alionekana akiwa ameshika tama na hata raha ya jina lake haikuwepo tena. Ilionyesha alitarajia ushindi ili aonyeshe "fedha ipo Jangwani", lakini wapi.
Baadhi ya waandishi walifika kumhoji wakiwepo wa kampuni ya Clouds FM.
BWANA ESCROW AKIHOJIWA NA WAANDISHI WA CLOUDS TV
Akaunti ya Tegeta Escrow imekuwa maarufu kutokana na taarifa za uchotwaji wa mamilioni ambao unaelezwa viongozi wakiwemo wa serikalini na hata wa dini wamegawana.
Ikulu ya Tanzania iansubiriwa kuhitimisha kuhusiana na suala hilo ambalo liko mikononi mwa Rais Jakaya Kikwete. 


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic