December 14, 2014

Mshambuliaji wa Simba, Elius Maguri alifunga bao la pili na kuipa ushindi timu yake wa mabao 2-0 dhidi ya Yanga akiwa amezungukwa na mabeki watano.


Mabeki wa tano wa Yanga walikuwa karibu ya Maguri wakati akiruka kupiga kichwa kutokana na mpira wa kurushwa wa Nassor Chollo.

Baada ya kuupiga mpira huo uligonga mwamba na kurudi lakini hakuna beki aliyekuwa ameokoa, hivyo akaruka na kuupiga tena kwa mguu na kufunga.
Wakati huo, mabeki hao walikuwa kama wamepigwa ganzi au watu wanaoshuhudia filamu.


Simba ilishinda kwa mabao 2-0 katika mechi hiyo iliyopigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic