December 17, 2014


Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) limeiagiza Etoile du Sahel kulipa kitita cha dola 300,000 (Sh milioni 480) pamoja na faini.
Fifa imeitaka klabu hiyo ya Sousse nchini Tunisia kuhakikisha inalipa fedha hizo ndani ya mwezi mmoja pamoja na faini ya dola 28.
OKWI (KUSHOTO) WAKATI AKIICHEZEA ETOILE KATIKA LIGI YA TUNISIA

Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) limeiagiza Etoile du Sahel kulipa kitita cha dola 300,000 (Sh milioni 480) pamoja na faini.



Fifa imeitaka klabu hiyo ya Sousse nchini Tunisia kuhakikisha inalipa fedha hizo ndani ya mwezi mmoja pamoja na faini ya dola 28,000.


Hatua hiyo imefikia baada ya Simba kushinda kesi iliyotokana na Simba kushitaki kwa Fifa baada ya Etoile kushindwa kulipa fedha za malipo ya kumnunua Emmanuel Okwi.

Okwi aliuzwa wakati wa uongozi wa Ismail Aden Rage na Etoile ikautumia mwanya huo kuanza kuizungusha Simba.

Rage aliahidi Etoile wangelipa wakati akiwa madarakani, kabla hajaondoka, lakini haikuwa hivyo.

Zigo likamuangukia yeye kwa kuwa ndiye aliidhinisha Okwi kwenda Etoile hata kabla ya Waarabu hao kulipa, kabla ya kumgeuka.

Etoile walizidi kusumbua baada ya Okwi kurejea Uganda na baadaye Yanga, hali iliyofanya Simba kukata tama.

Taarifa zinaeleza barua ya agizo hilo, tayari imetua TFF ambayo imewasilisha kwa Rais wa Simba, Evans Aveva kwamba anatakiwa kupokea mzigo pamoja na faini hiyo ndani ya mwezi mmoja.

Tayari Okwi ameisharejea Simba akitokea Yanga, hivyo Simba itafaidika kuwa na mchezaji halafu na mkwanja juu.


1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic