December 12, 2014


Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), limekaa leo na watani Simba na Yanga na kukubaliana upya.

Awali, TFF ilitangaza kuwa wachezaji ambao usajili wao umekamilika ndiyo pekee wataruhusiwa kucheza mechi ya Nani Mtani Jembe, kesho.

Lakini katika kikao cha leo, TFF imekubali (Kama Hoja ya Salehjembe ilivyoeleza leo), kuwa Simba na Yanga zinaweza kuwatumia wachezaji wao hata wale ambao hawajakamilisha usajili.

Uamuzi huo unaifanya Simba kupata nafasi kuwatumia wachezaji wachezaji wake kutoka Uganda kama sehemu ya majaribio.

"Kweli kikao kimemalizika, sasa tutawatumia wachezaji wote, hii ni kama majaribio na si lazima wawe wamesajiliwa," kilieleza chanzo.

Lakini Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Clement Sanga amesema wamekubaliana kuwatumia wachezaji hata ambao hawajasajiliwa.

"Ukiangalia sasa ndiyo dirisha dogo, hivyo ni mchezo mzuri kuwaangalia wachezaji, hivyo tutawatumia hata ambao hawajasajiliwa," alisema Sanga.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic