December 12, 2014

NAFASI YAKO, INACHUKULIWA NA HUYU BWANA: UNAWEZA KUDHANI KOCHA MARCIO MAXIMO ALIKUWA ANAMUELEZA HIVYO MSHAMBULIAJI HAMISI KIIZA WAKATI AKIZUNGUMZA NAYE PAMOJA NA MSHAMBULIAJI KPAH SHERMAN KUTOKA LIBERIA AMBAYE AMECHUKUA NAFASI YAKE.
Hatimaye safari ya Mganda Hamis Kiiza imewadia, kwa kuwa ametemwa.
Taarifa za kutoka ndani ya Yanga zinaeleza Kiiza ndiye ‘ametolewa’ kafara kwa nafasi yake kuchukuliwa na Kpah Sherman raia wa Liberia.

Sherman amesaini mkataba wa miaka miwili kuichezea Yanga.
Ili Yanga imtumie, imelazimika kumuacha Kiiza ili ipate nafasi moja.


Nafasi nyingine za wachezaji wa kimataifa zimejazwa na Haruna Niyonzima na Mbuyu Twite (Rwanda), Emerson na Coutinho (Brazil).

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic