December 16, 2014


Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppea amesema watani wao Yanga watafukuza sana makocha lakini hawataacha kuwapa kichapo.


Hans Poppe amesema Simba imekuwa na maandalizi ya kutosha, mipangilio mizuri katika usajili ndiyo maana imekuwa ikiendelea kuinyanyasa Yanga ifanyavyo.

"Watabadili sana makocha, sisi pia tutaendela kuwatandika tu.

"Hata huyu kocha waliyemrudisha (Hans van der Pluijm) anaijua kazi ya Simba. Sasa sijui kama atakuwa na jipya," alisema.

Yanga iko katika hatua za mwisho kumfungishia virago Kocha Marcio Maximo. Tayari kocha wake wa zamani, Pluijm amewasili jijini Dar es kumalizana na Yanga kabla ya kuanza kazi.

Msimu uliopita katika mechi ya Nani Mtani Jembe, Simba iliitwanga Yanga kwa mabao 3-1 na kusababisha kutimuliwa kwa kocha Ernie Brandts.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic