December 16, 2014

AKIWA NA RAIS WA SIMBA, EVANS AVEVA...
Kiungo mshambuliaji kwenye kasi, Emmanuel Okwi ameongeza mkataba na klabu hiyo kwa mwaka mmoja na klabu ya Simba maarufu kama Wanamsimbazi.
Mkataba wa Okwi sasa utamalizika mwishoni mwa msimu wa 2015-16.

Okwi amesaini mkataba huo mpya leo mbele ya Rais wa Simba, Evans Aveva na makamu wake, Geofrey Nyange ‘Kaburu’.
AKIWA NA MAKAMU WA RAIS WA SIMBA, KABURU...

Simba ndiyo klabu inayoshikilia rekodi nchini ya kuwa na wachezaji watano wa kigeni, wote kutokea katika taifa moja la Uganda.
Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe amesema wamemalizana na Okwi ambaye ameongeza mkataba huo.

"Okwi ameongeza mkataba wa mwaka mmoja na klabu aipendayo, zoezi limefanyika leo jijini Dar kama unavyoona picha," alisema Hans Poppe.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic