December 16, 2014

PLUIJM AKIWA NA MENEJA WA YANGA, HAFIDH SALEH ALIYEKWENDA KUMPOKEA KWENYE UWANJA WA NDEGE WA KIMATAIFA WA JULIUS NYERERE (JNIA) BAADA YA KUWASILI SAA NANE NA NUSU NA NDEGE YA SHIRIKA LA NDEGE LA ETHIOPIA.

Kocha Hans van Der Pluijm ametua jijini Dar es Salaam, tayari kuchukua nafasi ya Marcio Maximo.

Pluijm amewasili usiku wa kuamkia leo, lakini akakataa katakata kuweka wazi kwamba yuko tayari kuchukua nafasi hiyo.
GARI LILILOMBEBA PLUIJM LIKIONDOKA ENEO LA TUKIO...

Badala yake, Pluijm amesema amekuja nchini kwa ajili ya kufanya mazungumzo na uongozi wa Yanga.

“Ngoja nifanye mazungumza na uongozi wa Yanga, halafu tutaongea,” alisema.


Pluijm aliondoka Yanga kwenda Al Shaolah FC ya Saudi Arabia ambayo ilimzingua, akaamua kubwaga manyanga.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic