MBEYA CITY |
Yanga itabaki mjini
Bagamoyo kuendelea na kambi hata baada ya mechi dhidi ya Azam FC kesho.
Yanga ikimalizana na Azam,
itaelekea Mbeya kuumana na Mbeya City kwenye Uwanja wa Sokoine kisha kuivaa
Coastal Union kwenye Uwanja wa Mkwakani, Tanga.
Jerry Muro ambaye ni
mkurugenzi wa habari wa Yanga alisema kuwa wameamua kubaki Bagamoyo kulingana
na uzito wa mechi zilizo mbele yao, hivyo baada ya mechi hizo tatu benchi la
ufundi litalazimika kutoa tathmini yake kulingana na kambi hiyo kisha watatoa
mapendekezo yao mengine kulingana na mechi nyingine zinazofuata.
“Yaani kwa sasa programu
ndiyo ipo hivyo, timu ikimaliza mechi na Azam itarejea Bagamoyo na itadumu huko
mpaka imalize mechi zake za Mbeya na Coastal, tumeamua kubaki huko kutokana na
ugumu wa mechi zenyewe.
“Lakini baada ya mechi hizo
tutalisikiliza benchi la ufundi linasemaje na lina tathmini ipi kuhusiana na
kambi wanayoitaka kutokana na mechi zitakazokuwa mbele yao kwa wakati huo,”
alisema Muro.
0 COMMENTS:
Post a Comment