Kocha wa zamani wa Makipa wa
Simba, Idd Pazi yupo mbioni kutimkia nchini Oman kufundisha soka katika Timu
ya Do Sahel Lasalle, baada ya kutoelewana kimaslahi na timu ya Coastal Union ya
jijini Tanga.
Pazi aliachana na Simba
mwanzoni mwa msimu huu baada ya kumaliza mkataba wake ikiwa ni pamoja na
uongozi wa klabu hiyo kutoonyesha nia ya kumuongezea.
Pazi amesema kuna rafiki yake ambaye yupo Oman ndiye
anayemfanyia mpango wa kumtafutia timu ambapo yupo katika mazungumzo na Do
Sahel Lasalle ya nchini humo na mambo yatakapokamilika ataondoka wakati wowote.
“Mipango yangu ya sasa ni
kurudi Oman kwenda kufundisha soka ambapo kuna timu ya Do Sahel Lasalle ambayo
rafiki yangu ananitafutia nafasi na mipango ikikamilika tu naondoka,” alisema
Pazzi.
0 COMMENTS:
Post a Comment