December 13, 2014


SHERMAN...
SIMBA na Yanga zinatarajiwa kukutana kwenye Uwanja wa Taifa, leo katika mechi ya Nani Mtani Jembe 2, pamoja na kuwa kuna mambo mengi gumzo lakini moja kubwa ni juu ya wachezaji wa kimataifa wa timu hizo mbili, Kper Sherman wa Yanga na Emmanuel Okwi wa Simba.


Mastaa wote hao wanavaa jezi namba 25 kwenye timu zao, hivyo mashabiki wanasubiri kuona nani atamfunika mwenzake kwenye kipute hicho ambapo kila upande unavuta kwake.


Okwi:
Alitua Simba akiwa hana jina kubwa, akatengenezwa na kuwa staa akiwa anavaa jezi namba 25, akaondoka kwenda nje ya nchi, baada ya mizunguko ya hapa na pale akarejea nchini na kutua Yanga ambapo alivaa jezi namba 25 pia, akawa kipenzi klabuni hapo, lakini haukupita muda akarejea ‘nyumbani’.


 Sherman:
Jina lake limekuwa kubwa ghafla, ni mgeni kwenye soka la Tanzania na hajacheza mechi yoyote, lakini kwa waliofika mazoezini wamesema kuwa mbali na mwili mzuri wa soka lakini anaonyesha yupo fiti.

Hukumu

Wote ni washambuliaji, Okwi ni Mganda wakati mwenzake ni Mliberia, ni muda pekee ndiyo utakaothibitisha nani ni mkali zaidi kati ya mastaa hao wanaomiliki jezi namba 25.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic