December 11, 2014



Meneja wa Uwanja wa Taifa jijini Dar, Rish Urio amewaonya mashabiki wa Simba waliokuwa wana mpango wa kulala kwenye uwanja huo.

Baadhi ya wanachama na mashabiki wa Simba wakiongozwa na tawi la Mpira Pesa walitaka kwenda kuulinda uwanja huo, wakidai watani wao Yanga wana mpangowa kufanya ushirikina.

Yanga na Simba zinakutana keshokutwa Jumamosi katika pambano la kirafiki kwenye Uwanja huo.

“Kwa kweli hakuna atakayeruhusu watu kuja kulala na kulinda.
“Sisi tunaamini mpira ni maandalizi uwanjani, si suala la ushirikina.

“Hakuna atakayeruhusiwa kuingia uwanjani hadi siku ya mechi na hili ni msisisitizo,” alisema Urio.


“Ukisema kuhusiana na maandalizi, basi nakuhakikisha kila kitu kimekwenda poa kabisa”

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic