December 17, 2014

SHERMAN

Uwezo ulioonyeshwa na straika mpya wa Yanga, Mliberia, Kpha Sherman, kwenye mechi ya Nani Mtani Jembe pamoja na kwenye mazoezi ya timu hiyo, umemkosha kiungo Mnyarwanda, Haruna Niyonzima na kudiriki kusema: “Kweli sasa tumepata mtu mwenye kazi yake.”

NIYONZIMA

Sherman alitua nchini wiki iliyopita akitokea Cyprus alikokuwa anacheza soka la kulipwa, akasaini mkataba wa miaka miwili kuitumikia Yanga lakini ameteka hisia za mashabiki wa Yanga baada ya kuonyesha uwezo mkubwa kwenye mchezo wa wikiendi iliyopita dhidi ya Simba, ingawa walifungwa 2-0.

Niyonzima amesema kwa uwezo alionao Sherman, ni dhahiri anayaona mafanikio ya Yanga katika suala la kufunga kutokana na mchezaji huyo kujua zaidi anachotakiwa kufanya anapokuwa na mpira.

“Kwa kweli sasa hapa tumepata mtu anayeielewa sawasawa kazi yake, jamaa ana nguvu, anakaba, anajua nini cha kufanya anapokuwa na mpira au anapokuwa ameukosa, kwa kifupi ni mtu mwenye kujua majukumu yake.

“Kwa timu yetu ya Yanga ilivyo, naweza kusema kuwa ujio wake ndiyo suluhisho letu la kufumania nyavu kwenye mechi za hapa kwenye ligi ya nyumbani au hata za kimataifa, naweza kusema nimeufurahia kwa kweli ujio wake,” alisema Niyonzima. 


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic