December 17, 2014


Baada ya kuwa nje takribani misimu miwili mfululizo, hatimaye kiungo wa zamani wa Simba, Kiggi Makasi, amerejea rasmi uwanjani baada ya kusajiliwa na kikosi cha Ndanda FC na kuitumikia timu hiyo msimu huu kwa mwaka mmoja.


Kiungo huyo alikuwa akiitumikia Simba na alipata majeraha ambayo yalimweka nje baada ya kuumia katika mchezo wa kirafiki dhidi ya CDA ya Dodoma na baadaye kupelekwa India kufanyiwa upasuaji na hakuweza kurejea tena uwanjani.

Msemaji wa timu hiyo, Idrissa Bandari, alisema anaamini atakuwa na mchango mkubwa katika kikosi chao ndiyo maana wamemsajili.

Kiungo huyo alifanya vyema katika timu ya taifa kipindi cha Mbrazili, Marcio Maximo, alipokuwa akiitumikia Simba.

“Natumai atakuwa na msaada mkubwa katika timu yetu kwa sababu ni mzoefu, ndiyo maana kocha kaamua kumuongeza baada ya kuona uwezo wake ni mzuri,” alisema Bandari.

Kwa upande wake kiungo huyo, alisema: “Nashukuru kwa sasa nipo fiti zaidi, nitajituma ili kuweza kusaidia timu yangu kufanya vizuri kwa kushirikiana na wenzangu.”


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic