Suala la kipa wa Yanga, Juma
Kaseja linaendelea kuzunguka ndani ya Kamati ya Nidhamu ya Yanga, hata hivyo kuna taarifa kuwa bado kipa huyo mkongwe atakatwa mshahara.
Imeelezwa kuwa jina la
Kaseja limepelekwa kwenye kamati hiyo kutokana na kugoma kufanya mazoezi na
kikosi hicho baada ya kuwepo migogoro ya hapa na pale lakini kubwa ni kuhusu
malipo ya fedha zake za usajili alizokuwa akidai.
Taarifa nyingine zinasema Kaseja hakuwa amekataa kufanya mazoezi lakini amekuwa hajibiwi barua zake baada ya suala la kuchelewa kumlipa lilianzisha mgogoro kwisha.
Kutokana na hilo, hata
baada ya kuelezwa kuwa pande mbili hizo zimeshakamilishiana malipo hayo lakini
Yanga ikamwekea ngumu kurudi mazoezini mpaka suala lake litakapokwisha kwenye
kamati ya nidhamu, lakini hapo hapohapo ndiyo likaibuka hili la mshahara.
Ofisa Habari wa Yanga,
Jerry Muro ameliambia Championi Jumamosi kuwa Yanga ina taratibu zake kwa
mchezaji anayekosa kuhudhuria mazoezini na kwenye mechi bila ya sababu maalum,
hivyo adhabu yake katika hilo bila ya kujadiliwa mahala popote ni kumkata
mshahara mchezaji huyo.
“Yaani mchezaji asipokuja
mazoezini bila sababu maalum hiyo inakuwa ni tatizo zaidi kwa upande wake kwa
sababu inaeleweka hata kama suala lisipofika kujadiliwa kwa uongozi lazima
mchezaji atakatwa mshahara na hilo lipo wazi na linaeleweka.
Tangu Yanga ianze mazoezi
Novemba 24, mwaka huu kwa ajili ya kujiandaa na ligi kuu raundi ya nane, Kaseja
amekuwa akikosekana mazoezini mpaka yale ya mwisho ya timu hiyo yaliyofanyika
Jumatano kwenye Uwanja wa Boko Veterani, Ununio, nje kidogo ya Dar.
0 COMMENTS:
Post a Comment