Kocha Hans van der Pluijm wa Yanga amesema
mmoja wa wachezaji wanaomvutia zaidi ni kiungo Haruna Niyonzima.
Pluijm raia wa Uholanzi amesema Niyonzima ni
mmoja wa viungo bora kabisa katika ukanda wa Afriak Mashariki.
Akizungumzia kuwepo na taarifa za
kutoridhishwa na kiwango cha Niyonzima, Pluijm amesema, haijawahi kutokea.
“Niyonzima amekuwa mmoja wa wachezaji
wanaonipa ushirikiano mkubwa. Kama utakuwa umesikia habari hizo, basi ni maneno
tu.
“Kocha wa aina gani anaweza kusema Niyonzima
si kungo bora. Tena anaweza kucheza nafasi zaidi ya moja,” alisema.
Niyonzoma raia wa Rwanda ni kati ya viungo
wazoefu wanaounda safu ya ‘upikaji’ ya Yanga.
0 COMMENTS:
Post a Comment