December 16, 2014


Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limepokea kwa masikitiko taarifa za kifo cha Kocha Mshindo Madega kilichotokea leo (Desemba 16 mwaka huu) mjini Bukoba.


Mbali ya kuwahi kuwa mchezaji katika timu ya RTC Kagera, Kocha Madega aliwahi kufundisha timu za Kagera Stars, Mwadui na kombaini ya Copa Coca-Cola ya Mkoa wa Kagera.

Mchango wake katika mchezo wa mpira wa miguu tangu akiwa kocha na baadaye kocha utakumbukwa daima.

Tunatoa salama za rambirambi kwa familia ya marehemu, Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Kagera (KRFA), Chama cha Makocha wa Mpira wa Miguu Tanzania (TAFCA) Mkoa wa Kagera na klabu ya Bukoba Veterans na kuwataka kuwa na subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha msiba huo.

TFF itawakilishwa kwenye msiba huo na Chama Soka Mkoa wa Kagera (KRFA).


1 COMMENTS:

  1. i ni nana mie rehrehzma za kuni ongoza na utimilifu hata hapa na mashaka na magonjwa raihisi magufuli afungue namaengelezi za suu sisi na vijana waze she gari na vifa vya kuponyesha nasizani kama kuna vifa huko nunua jembe hata cooplo ina tibika je kuhishiwa damu na maji kwenye mkojo na kikipima damu na kutembelea sehemu kuu huku mqatibabu wapombe waache tusi potezane

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic