December 11, 2014


Baada ya kuzingua vya kutosha, hatimaye nahodha wa Unaweza ukadhani utani lakini huu ndiyo ukweli kwamba kwa sasa Simba ina wachezaji Waganda watano.


Sheria za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ni wachezaji watano wa kigeni, Simba inao saba.
Waganda watano na Warundi wawili na wote wako kwenye kambi ya timu hiyo iliyo Zanzibar.
MURSHID
Waganda wawili, Juuko Murshid na Joseph Sserunkuma wametua jana kwa ajili ya majaribio. 
Iwapo Simba itataka kuwasajili, sasa itakuwaje? Kama itawakubali Murshid na Joseph, basi Warundi watalazimika kuondoka.
SSERUNKUMA

Kumekuwa na taarifa kwamba, Simba inaona bora kuachana na Owino na kumtwaa Murshid. Lakini bado Simba wanapaswa kujiridhisha kumuona Murshid kwanza.

Ila kama Simba itawakubali Murshid na Joseph, basi itakuwa ni rekodi mpya ya kusajili wachezaji wote wa kigeni kutoka nchi moja ya Uganda.

WAGANDA:
 1. Joseph Owino
2. Emmanuel Okwi
3. Dan Sserunkuma
4. Juuko Murshid
5. Joseph Sserunkuma

WARUNDI:
1. Pierre Kiongera
2. Amissi Tambwe


3 COMMENTS:

  1. Sidhani kama kuna taarifa yoyote rasmi au ya uhakika kuwa simba ina mpango wa kukata wachezaji wawili. Habari zinazosikika sana ni kuwa wanataka beki mmoja tu, hivyo basi wanaweza wakamkata mchezaji mmoja. Simba haina mchezaji Mrundi anayeitwa Pierre Kiongera, ila yupo mrundi anayeitwa Pierre Kwizera na pengine ndiye atakayekatwa. Na kwa maoni yangu Kwizera si kiungo mbaya hasa kama Mkude ataumia au atahitaji msaada. Anahitaji mechi zaidi kudhihirisha ubora wake. Ni bora hata kumkata tambwe kwa kuwa kuna maguri, okwi na sserunkuma kuliko kwizera

    ReplyDelete
  2. Simba wanajichanganya wenyewe,sasa wachezaji wote hao wa nini,waache tamaa ukizingatia hivi sasa ni msimu wa usajiri wa dirisha dogo,iwapo hao warundi wakigoma kukatwa watafanyaje au ndo watakuwa wametupa pesa zao bure tu.

    ReplyDelete
  3. Kwizera aende tu. Tunahitaji beki m1 wa kati. Na mwalimu nae asitumie mfumo m1 tu throughout. Atumie mifumo mingine si kila siku 4-4-2 tu. Aangalie atleast mfumo wa kum accomodate Tambwe angalau mechi 2 aone impact yake. Tambwe bado ni mfungaji mzuri tu. Namba ya kwizera ina watu wengi Awadh Juma anacheza pia

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic