Klabu ya Arsenal ya Uingereza, ipo kwenye mazungumzo na baadhi ya makampuni ya hapa
kwa ajili ya kujenda mahusiano ya kibiashara mbalimbali za vifaa zikiwemo jezi.
Akizungumza
na Waandishi wa Habari, Ofisa Biashara wa klabu hiyo, Sam Stone alisema kuwa
leo wanatarajia kukutana na makampuni mbalimbali kati ya 20 kwa ajili ya kujadiliana
masuala mbalimba ya kibiashara.
Stone
alisema, biashara waliyopanga kuifanya ni kuuza jezi zao orijino wanazozitumia
kwenye msimu, traki suti, soksi, viatu na vitu vifaa vingine vinavyohusiana na
michezo vya Arsenal.
“Tupo
hapa nchini kwa ajili ya kujenga mahusiano mazuri ya kibiashara kati ya hapa
nchini na klabu ya Arsenal, hivi sasa tupo kwenye mazungumzo na baadhi ya
makampuni tutakayofanya nayo kazi pamoja katika kuziuza jezi zetu orijino kwa
njia ya mtandano.
“Mpango
unaohusisha nchi za Afrika kwa hivi sasa, tulianza na Kenya, Uganda, South Afrika, Nigeria, Misri, Nigeria na hivi
sasa Tanzania,”alisema Stone.
0 COMMENTS:
Post a Comment