KATIKA PASI ZAIDI YA 2000 ZILIZOPIGWA KATIKA MECHI ZA LIGI KUU ENGLAND WIKI HII, ILIYOVUTIA ZAIDI NI ILE ALIYOPIGA KIUNGO ALEX SONG WA WEST HAM UNITED AKIMPA DOWNING AMBAYE ALIFUNGA BAO LA TATU DHIDI YA HULL CITY.
PASI HIYO ILIPIGWA UMBALI WA YADI 55 IKIWAPITA WATU KATIKATI KABLA YA KUMFIKIA MFUNGAJI AMBAYE ALIKIMBIA NAYO HATUA KADHAA KABLA YA KUFUNGA BAO HILO LA TATU.
SONG AMEACHWA KATIKA KIKOSI CHA TIMU YA TAIFA YA CAMEROON KWA MADAI YA UTUKUTU NAYE KWA HASIRA AMEAMUA KUTANGAZA KUSTAAFU KUCHEZA SOKA LA KIMATAIFA. |
0 COMMENTS:
Post a Comment