January 19, 2015

DOMAYO (KULIA) WAKATI AKIWA YANGA...
Baada ya kufanikiwa kuing’arisha Azam FC kwenye mechi ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Stand United juzi, kiungo mahiri Frank Domayo ametamba kuwa ndiyo anaanza kazi na moto wake utaonekana tu.


Domayo ambaye amerejea hivi karibuni kufuatia majeraha ya goti yaliyomweka nje kwa takribani miezi saba, alianza kung’aa kwenye Kombe la Mapinduzi na juzi aliifungia Azam bao pekee lililoipa ushindi dhidi ya Stand kwenye Uwanja wa Kambarage, Shinyanga.

Domayo alisema kuwa yeye hapendi kuongea maneno mengi ila ubora wake utazidi kuonekana pindi atakapozidi kucheza.

 “Soka haliongelewi kwa mdomo, ila ni kwa vitendo pekee, hasa pale unapokuwa uwanjani uwezo wako ndiyo unaonekana.


“Malengo yangu ni kuhakikisha nafanya vizuri ili kuibuka mfungaji bora msimu huu, japokuwa nimechelewa kuanza ligi kutokana na kuwa majeruhi, ila nitahakikisha najitahidi kadiri niwezavyo kurudisha heshima yangu,” alisema Domayo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic