January 19, 2015


Kweli nyumbani ni nyumbani baada ya mshambuliaji wa Mtibwa Sugar, Mussa Hassan Mgosi kuonyesha mapenzi yake wazi kwa klabu ya Simba.


Juzi Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar, Mgosi, aliwaacha wachezaji wenzake na kukaa mbali wakati kikosi kizima cha timu hiyo kilipoingia uwanjani hapo kushuhudia mchezo wa Ligi Kuu Bara kati ya Yanga na Ruvu Shooting.

Wachezaji wa Mtibwa waliweka kambi jijini Dar mara baada ya kutoka Zanzibar walipokuwa wanashiriki michuano ya Kombe la Mapinduzi iliyoisha Jumanne ya wiki iliyopita ambapo walimaliza katika nafasi ya pili.

Mtibwa ilikuwa na mechi siku inayofuata, yaani jana dhidi ya JKT Ruvu, hivyo siku wachezaji wake walikuwa 'free' siku hiyo.

Waliingia Taifa wakiwa wamevaa sare za timu yao na kukaa kwenye jukwaa la VIP A lakini  kwa Mgosi akaamua kuvua sare hizo na kuhamia jukwaa la rangi ya bluu, upande wa Kaskazini Magharibi ambao kawaida hukaa mashabiki wa Simba.

Alikaa upande huo na kushuhudia mechi hadi mwisho na baadaye akarudi na kuungana na wenzake.

Mgosi aliichezea Simba kwa mafanikio makubwa misimu mitano iliyopita na alikuwa mshambuliaji tegemeo na tatizo kubwa kwa wapinzani wao Yanga.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic