January 19, 2015


Mbeya City wameanza tambo kufuatia kushinda mechi mbili mfululizo kwenye Ligi Kuu Bara.


Uongozi wa timu hiyo ambayo baada ya mapumziko iliifunga Ndanda bao 1-0 mjini Mbeya, kisha juzi ikaifunga Kagera 1-0 ugenini kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, umetamka kuwa sasa upo kwenye mikakati ya kuhakikisha wanamaliza ligi ndani ya nafasi tatu za juu.

Mbeya City ilikwenda mapumziko ikiwa ya mwisho kwenye msimamo lakini sasa inashika nafasi ya 11.

Msemaji wa timu hiyo, Dismas Tena, alisema: “Kwa sasa tuna mipango maalumu ya kuhakikisha tunafanya juhudi za kuweza kurudi katika nafasi tatu za juu kama tulivyofanya msimu uliopita.


“Na tuna uhakika jambo hilo litatimia kutokana na ubora wa kikosi tulichonacho ambacho wachezaji wanajituma katika kila mchezo kuhakikisha tunaibuka na ushindi.”

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic