Kikosi cha Kagera Sugar kimetamba kuwa kitatembeza kipigo kwa Mbeya City Jumamosi ijayo kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza
katika mchezo wa Ligi Kuu Bara.
Kagera wamesema wao ni timu bora kuliko Mbeya
City ambao walikuja kwa mbwembwe msimu uliopita lakini msimu huu wameshindwa
kuonyesha makali yao.
Mtanange huo unachezwa Mwanza kwa kuwa Uwanja
wa Kaitaba wa mjini Bukoba unaotumiwa na Kagera unafanyiwa ukarabati.
Msemaji wa Kagera, Mohamed Hussein, amejigamba kuwa Mbeya City itegemee kipigo kikali kwa kuwa timu hiyo ni zaidi yao kutokana
na kupanda ligi kuu tangu msimu wa 2005/06 na haijawahi kushika mkia.
“Mbeya City ni timu kama timu nyingine za
Simba na Yanga ambazo tulizichapa na yenyewe isubiri kipigo kitakatifu kwa kuwa
ni timu changa kwetu kwani tumepanda daraja tangu msimu wa 2005/06 bila ya
kushika mkia hata mara moja tofauti na wao ambao wamepanda juzi tu lakini leo
tayari wameanza kutetereka.
“Kikosi chetu kipo vizuri na kwa sasa tupo
kambini kwa ajili ya kujiandaa na mchezo huo,” alisema Hussein.
0 COMMENTS:
Post a Comment