January 19, 2015

Mabeki wa Ruvu Shooting wamemtaja mshambuliaji wa Yanga, raia wa Burundi, Amissi Tambwe kuwa ndiye mchezaji tishio katika kikosi cha timu hiyo kwa kile walichodai kuwa anajua majukumu yake anapopata nafasi ya kufunga.
Hali hiyo ndiyo hasa iliyowafanya wamchunge zaidi kuliko mchezaji mwingi wa Yanga katika mechi yao ya juzi Jumamosi ya Ligi Kuu Bara iliyopigwa Uwanja wa Taifa, Dar na kumalizika kwa suluhu.

Beki wa kati wa Ruvu Shooting, George Michael Osei, alisema kabla ya mechi hiyo, kocha wao mkuu, Tom Olaba, aliwaambia kuwa mtu wa kuchungwa zaidi katika mechi hiyo ni Tambwe, hivyo kila mchezaji atumie mbinu yoyote ile kumwondoa mchezoni.

Alisema ndiyo maana baada ya kuanza kwa mechi hiyo, wachezaji wote wa timu hiyo walitumia mbinu hiyo kwa kuwagongagonga wale wa Yanga na mwisho wa siku wakafanikiwa kuwaondoa mchezoni.

“Tusingefanya hivyo hakika Tambwe lazima angetufunga, kwani ni mshambuliaji mjanja sana anapokuwa ndani ya eneo la hatari, hivyo bila ya kuwa makini angetuumiza.

“Washambuliaji wengine wa Yanga ni wa kawaida sana na hawana utulivu wanapopata nafasi za kufunga, ndiyo maana walikosa nafasi nyingi za kufunga tofauti na Tambwe ambaye alipata mbili, moja alifunga kwa mkono na mwamuzi akalikataa bao hilo lakini pia alipiga shuti kali ambalo lilituogopesha wote,” alisema Osei.


1 COMMENTS:

  1. Watu wanajisifia ujinga walioufanya uwanjani,na picha zinaonyesha
    lakini cha kushangaza TFF wanalifumbia macho.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic