Unaweza ukaona kama haiwezekani kwamba soka pia ni mchezo hatari na hilo limejidhihirisha katika mechi ya Ligi Kuu Bara kati ya Azam FC dhidi ya Simba.
Daktari amesema, moyo wa mshambuliaji Emmanuel Okwi
ulisimama kwa sekunde kadhaa alipogongwa kisogoni na beki Aggrey Morris wa Azam
FC. Maana yake kitafsiri, hiyo ni nusu kifo.
Okwi aligongwa katika mechi ya Ligi Kuu
Bara dhidi ya Azam FC iliyomalizika kwa sara ya bao 1-1 kwenye Uwanja wa Taifa
jijini Dar es Salaam, jana.
Daktari wa Simba, Yassin Gembe amesema moyo
wa Okwi ulisimama kwa sekunde kadhaa kutokana na pigo la kisogoni karibu kabisa
na ubongo katika eneo la Medullar Oblangata.
“Hakikuwa kitu kidogo, tulilazimika kufanya
tiba ili kurudisha mapigo ya moyo wake. Aliumia na uliona akitoa mapovu. Ndiyo maana uliona tulikuwa tukimkandamiza kwenye kifua ili kuamsha tena mapigo yake ya moyo upya.
“Baada ya hapo, tuliona ni jambo la msingi kumfikisha
Muhimbili ambako vipimo vyote vimefanyika. Imeonekana hakuumia sana na
ameruhusiwa.
“Lakini mimi nimeamua kumpumzisha kwa siku
mbili ili kuangalia kama atakuwa katika hali gani maana mwanzo unaweza kuona
yuko vizuri kumbe kuna tatizo.
“Ikionekana anaendelea vizuri, basi ataana
mazoezi lakini zoezi na atakuwa chini ya uangalizi wangu,” alisema Dk Gembe.
Mshambuliaji wa Simba, Danny Sserunkuma
alitumia muda mwingi kumlaumu Morris kwamba alishiriki kumpiga Okwi kiwiko,
hata hivyo alikuwa akikanusha.
Okwi alibebwa haraka na kutolewa uwanjani
na baadaye kukimbizwa Muhimbili ikiwa ni baada ya kuzinduka.
Kugongwa huko kwa Okwi, jana jioni kulizua
gumzo kwa mashabiki wa soka nchi hasa wa Simba ambao walikuwa wakipiga simu
katika ofisi za gazeti hili wakidai mabeki wamekuwa wakatili kwa washambuliaji.
Wengi walitolea mfano wa beki George
Michael wa Ruvu Shooting kumkaba mshambuliaji Amissi Tambwe wa Yanga.
0 COMMENTS:
Post a Comment