Klabu ya Yanga imechukua uamuzi wa
kuwashitaki wachezaji watatu moja kwa moja kwenye Shirikisho la Soka la
Kimataifa (Fifa).
Yanga imetangaza kuwashitaki kipa Juma
Kaseja, kiungo Mganda Emmanuel Okwi na mshambuliaji Jaja raia wa Brazil.
Mkurugenzi wa Sheria wa Yanga, Frank Chacha
amesema leo wamechukua uamuzi huo kutokana na wachezaji hao kukiuka vifungu vya
sheria.
“Lakini pia tutaishitaki Simba kwa kuhusika
kuvunja vifungu vya kisheria
kutokana na kumshawishi Okwi kuvunja mkataba wetu,” alisema Chacha.
Jaja:
Yanga inasema alishindwa kurejea nchini kwa
madai ana matatizo ya kifamilia. Lakini wanashangazwa kuwa hajarudi hadi leo na
kuna taarifa amepata timu nyingine, hivyo wanashitaki.
Okwi:
Amekiuka sheria kwa kuvunja mkataba,
wanaamini hakuwa sahihi na pia Simba ilimshawishi kuvunja mkataba nayo
wanaishitaki.
Kaseja:
Alishindwa kufuata vipengele vya kikatiba
ikiwa ni pamoja na kutokwenda mazoezini wanadai bila ya kuwa na taarifa yoyote.







0 COMMENTS:
Post a Comment