February 24, 2015


Ili kupisha hali ya kewa ya joto, michuano ya Kombe la Dunia iliyopangwa kufanyika nchini Qatar mwaka 2022 itapigwa kuanzia Novemba hadi Desemba.


Kwa kawaida michuano hiyo hufanyika kati ya miezi ya Juni la Julai.

Lakini kutokana na hali ya hewa ya nchi hiyo ya barani Asia kufikia hadi nyuzi joto 40 katika miezi ya Juni na Julai, Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) limelazimika kukwepesha.

Majibu hayo yametolewa baada ya kamati ya utendaji ya Fifa kukutana jijini Zurich, Uswiss kuanzia Machi 19 hadi 20.


Uamuzi huo unaondoa ndoto ya nchi za Ulaya kuwania kuipata nafasi hiyo kwa madai hali ya hewa ya Qatar si sahihi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic