February 6, 2015


Kocha Mkuu wa Mwadui, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ amefunguka kuwa kwa sasa kiwango chake cha ukocha siyo cha kuwa msaidizi tena hapa nchini na kama kuna timu itamhitaji lazima ikubali awe kocha mkuu.


Kauli hiyo inakuja kukiwa na tetesi kuwa Kocha Msaidizi wa Simba, Selemani Matola yupo mbioni kuondoka klabuni hapo na hivyo, msaidizi wa Goran Kopunovic anahitajika.

Julio ambaye ni mchezaji na kocha wa zamani wa Simba, amesema kuwa kama atahitajika klabuni hapo, uwezo wake ni kuwa kocha mkuu nafasi inayoshikiliwa na Kopunovic na siyo kuwa msaidizi kwa mara nyingine.

“Kwa sasa nina sifa zote za kuwa kocha mkuu na siyo kocha msaidizi, ndiyo maana nipo na timu yangu hii, hata kama ipo daraja la kwanza nina uwezo wa kuwa kocha mkuu Simba, Azam, JKT Ruvu na popote pale lakini siyo usaidizi tena,” alisema Julio ambaye alidai ana Leseni A ya ukocha ya Shirikisho la Soka la Afrika (Caf).

“Naamini naweza kufundisha mahali popote na sichagui iwe ligi kuu au daraja la kwanza kwa sababu ni profesheno yangu na ndiyo maana nimejiendeleza na kuweza kufika hapa na kuwa mwalimu bora,” aliongeza Julio.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic