Ile ishu ya kiongozi mmoja wa Simba kuzuiwa kuingia kambini, imezidi kuchukua sura mpya. Hii ni baada ya Makamu Mwa Simba, Geofrey Nyange ‘Kaburu’
kufunguka baada ya kuwa na taarifa kuwa yeye ndiye mlengwa.
Hivi karibuni vyombo
mbalimbali vya habari vimekuwa vikiripoti kuwa kuna kiongozi amekatazwa
kuitembelea kambi ya timu hiyo kutokana na kuhusishwa kumpangia kocha timu.
Baadhi ya vyombo vya habari
vilimtaja kiongozi huyo ambaye amefungukia ishu hiyo.
Kaburu ambaye pia ni Mjumbe
wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), amesema kwamba
taarifa hizo hazimhusu yeye kwa kuwa yeye kwanza hana tabia ya kwenda kambini
na pia hilo si jukumu lake, hivyo si kweli kwamba yeye ndiyo mlengwa wa kuzuiwa
huko.
Alifafanua kuwa yeye ana
majukumu yake ndani ya timu hiyo na si ya kuitembelea timu inapokuwa kambini
kwa kuwa watendaji wa masuala hayo wanajulikana na pia kama ingekuwa
amesimamishwa kwa mujibu wa taratibu zilivyo, ni lazima angeitwa na kuambiwa
hata katika kikao chao cha viongozi.
“Sijazuiwa na wala
sijaambiwa chochote kuhusu mambo ya kwenda au kutokwenda kambini kwa sababu
kwanza mimi si mtu wa kwenda kambini mara kwa mara kwa ajili ya kuitembelea
timu, isipokuwa huwa nakwenda huko kama inatokea kuna kikao cha viongozi na
timu nzima.
“Kama ingekuwa ni kweli
nimezuiwa kufika baadhi ya sehemu na uongozi basi ningeambiwa tu lakini mpaka
sasa sina taarifa yoyote, kwa hiyo ina maana si mimi mlengwa wa suala hilo,
mimi kazi yangu ni majukumu ya kiofisi tu na si mengine kama hayo ninayoambiwa
kuwa nimekatazwa kufika kambini.
“Pia hizi taarifa za
kumpangia kocha kikosi si za kweli, mimi siwezi kufanya hivyo kwa kuwa hiyo si
kazi yangu, ni kazi ya kocha, kocha ameletwa kwa ajili ya kazi hiyo kwa hiyo
siwezi kumuingilia kwenye majukumu yake.
"Ila naweza kupiga stori na kocha
kuhusu wachezaji aliowachezesha na kumuuliza kwa nini alimchezesha huyu na kumuacha
yule, basi, na si vingine, na hiyo kuzungumza na mwalimu kuhusu masuala hayo si
kumpangia kikosi ila ni kama unahitaji kujua tu,” alisema Kaburu.
0 COMMENTS:
Post a Comment