February 25, 2015


Wachezaji watano wa Mtibwa Sugar, tena wale muhimu, mikataba yao imefikia tamati na wamegoma kuongeza mipya!

Nyota wanaotajwa kutangaza nia ya kuondoka ni kipa tegemeo Said Mohammed, Salim Mbonde na Henry Joseph Shindika, ambaye alisaini miezi sita katikati ya msimu huu baada ya kuachana na Simba mwishoni mwa msimu uliopita.

Habari za kina zinasema kuwa, Mohammed yupo mguu ndani-nje kujiunga na mabingwa watetezi, Azam, Mbonde anawindwa na Simba huku Shindika yeye akifunguka mwenyewe kuwa kwa sasa hawezi kuongeza mkataba mwingine hadi msimu umalizike huku akikaribisha timu yoyote.

“Mkataba wangu unaisha na bado sijafanya mazungumzo na mtu yeyote mpaka sasa, hata hivyo sipo tayari kwa kipindi hiki. Nasikilizia kwanza upepo wa dili kwenye usajili, unajua unaweza kupata dili la maana kwenye kipindi cha usajili. Iwapo kutakuwa na timu inanitaka, basi niko tayari kuisikiliza hata sasa hivi,” alisema nyota huyo wa zamani wa Simba na Taifa Stars.

Msemaji wa Mtibwa, Thobias Kifaru, alikiri kuwepo kwa dalili za nyota wao kutaka kuondoka lakini akasema watakaa chini kuzungumza nao.

“Kwa sasa timu inaonekana kupooza kabisa, nafikiri ni kutokana na matokeo mabaya, lakini wajue ni upepo tu unapita, kesho keshokutwa tutakaa sawa, suala la msingi tutakaa nao kuangalia jinsi ya kuboresha mikataba yao,” alisem Kifaru.


Timu hiyo imeambualia pointi moja katika mechi tano za hivi karibuni na kushushwa kutoka kileleni hadi nafasi ya sita kwenye msimamo wa ligi kuu, ambayo inaongozwa na mabingwa wa kihistoria, Yanga.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic