February 23, 2015


Kocha Mkuu wa Simba, Mserbia, Goran Kopunovic, amemtaka kipa Hussein Shariff ‘Casillas’ kuhakikisha anakuwa fiti wakati anajiunga na kikosi chake.


Kipa huyo, alijiunga na Simba katika usajili wa mwanzoni mwa msimu huu akitokea Mtibwa Sugar. 

Alisaini mkataba wa miaka miwili lakini amekuwa akikumbwa na majeraha ya mara kwa mara.

Katibu Mkuu wa Simba, Stephene Ally, alisema kocha huyo hana shida na kipa huyo, kikubwa anamtaka awe fiti kabisa kabla hajaingia kwenye kikosi cha kwanza.

 “Kopunovic yupo tayari kufanya kazi na Casillas, lakini kocha ametoa sharti kwamba kama kipa huyo anataka kurejea kikosini, basi awe amepona kabisa na fiti kwa ajili ya ligi kuu.

“Kikubwa kocha anataka kuwa na mchezaji ambaye yupo fiti, siyo majeruhi. Ni kama ilivyokuwa kwa Owino (Joseph) ambaye alipona kabisa ndiyo akamrejesha kikosini,” alisema Stephene.

Kocha huyo, hivi karibuni alitangaza kuwa hana kipa namba moja kwenye kikosi chake, kati ya Ivo Mapunda, Peter Manyika na Casillas mwenyewe.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic