February 23, 2015

Cristiano Ronaldo amekuwa mchezaji wa tatu mwenye uwezo wa ‘kudungua’ katika kikosi cha Real Madrid.


Ronaldo ameshika nafasi hiyo ya tatu nyuma ya magwiji wawili, Raul Gonzalez na Alfredo Di Stefano baada ya kufunga bao moja katika mechi waliyoshinda kwa mabao 2-0 dhidi ya Elche.

Katika mechi hiyo, Karim Benzema alitangulia kufunga katika dakika ya 56 kabla ya Ronaldo kufunga la pili.

Pamoja na kuwa mkali wa mabao, Ronaldo pia anashkilia tuzo tatu za Ballon d'Or, moja aliipata akiwa Man United mwaka 2008 na mbili baada ya kutua Real Madrid.

WAFUNGAJI BORA WA REAL MADRID
Raul: Mabao 323, Mechi 741
Alfredo Di Stefano: Mabao 307, Mechi 392
Cristiano Ronaldo: Mabao 290, Mechi 281
Carlos Santillana: Mabao 290, Mechi 645
Ferenc Puskas: Mabao 242, Mechi 262




0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic