Timu ya Taifa ya Tanzania ya Sola la Ufukweni (Beach Soccer)
iliyoingia kambini mwishoni mwa wiki Bamba Beach Kigamboni, inaendelea na
mazoezi kujiandaa na mchezo dhidi ya timu ya Taifa Soka la Ufukweni ya Misri mwishoni
wiki ijayo.
Maandalizi ya mchezo dhidi ya timu ya Misri yanaendelea vizuri
Bamba Beach Kigamboni chini ya kocha mkuu John Mwansasu ambaye aliingia kambini
mwishoni mwa wiki na wachezaji 14.
Mchezo wa kwanza unatarajiwa kufanyika Ijumaa ya Machi 13 katika
klabu ya Escape 1 Msasani jijini Dar es salaam na marudio yake kufanyika
baada ya wiki moja nchini Misri.
Tanzania ilifanikiwa kufuzu hatu ya pili baada ya kuitoa timu ya
Taifa ya Kenya kwa jumla ya mabao 12- 9, mchezo wa awali Mombasa Tanzania ilishinda
kwa mabao 5-3, na mchezo wa marudiano uliofanyika klabu ya Escape 1 kuibuka na
ushindi wa mabao 7-6.
Fainali za Mataifa Afrika kwa Sola la Ufukweni (Beach Soccer)
zinatarajiwa kufanyika mwezi April 2015 katika Visiwa vya Shelisheli.
0 COMMENTS:
Post a Comment