Kiungo Mbrazil, Andrey
Coutinho ameeleza wazi namna goti linalomuuma linavyomchanganya.
Coutinho ni majeruhi na
dalili zote zinaonyesha ataikosa mechi dhidi ya Platinum ya Zimbabwe, Jumapili.
Hali hiyo inamfanya azidi
kuwa na hofu ya kuendelea kubaki benchi licha ya juhudi kubwa za Yanga
kuhakikisha anarejea.
“Bado, lakini naendelea
kupata matibabu. Goti linanibakiza nje na mimi sipendi kukaa benchi,” alisema
Coutinho.
“Huenda hivi karibuni mambo
yakawa mazuri, nitafurahi nikirejea,” aliongeza.
Katika mazoezi ya leo ya
Yanga, Coutinho aliendelea kukaa nje akishuhudia wenzake wakikitimua na baadaye
alifanya mazoezi mepesi kabisa.







0 COMMENTS:
Post a Comment