March 13, 2015


Kocha wa Mtibwa Sugar, Meck Maxime amesema wana imani ya kufanya vizuri dhidi ya Simba kesho.


Maxime amesema wamejiandaa vilivyo na kinachotakiwa kwao ni kujiamini na kupambana.

“Unakumbuka tumepita katika wakati mgumu sana lakini hakuna aliyekata tamaa.


“Kamwe hatujawahi kuwadharau Simba. Hata mechi ya mzunguko wa kwanza tulisema wamecheza vizuri na tukatoka sare.

“Tunajua watakuwa nyumbani, lakini mpira wa sasa haujali ugenini au nyumbani, tutapambana,” alisisitiza.


Simba inashuka dimbani Uwanja wa Taifa, Dar, kesho kuwavaa Mtibwa katika mechi ya Ligi Kuu Bara.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic