March 17, 2015


Mechi ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika kati ya Yanga dhidi ya FC Platinum ya Zimbambwe kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, Jumapili imeingiza Sh 91,660,000.


Kitita hicho cha Sh milioni 91 kimetokana na watazamaji 14,563 waliokata tiketi kushuhudia mchezo huo.

Yanga iliwakung'uta Wazimbabwe hao kwa mabao 5-1 katika mechi hiyo ya kwanza ya Kombe la Shirikisho.

Mgawanyo: 
Mgawanyo wa mapato katika mchezo huo ni, VAT 18% Sh 13,982,033, Gharama ya tiketi Sh 12,380,000, Uwanja 15% Sh  9,794,694.92, Gharama za mchezo 15% Sh  9,794,694.92, TFF 5% Sh  3,264,898.31, CAF 5% Sh  3,264,898.31 na Yanga 60% Sh 39.178,779.66 (baada ya 18% ya vat kuondolewa).


IMETOLEWA NA MSEMAJI SHIRIKISHO LA SOKA TANZANIA (TFF), BARAKA KIZUGUTO.

2 COMMENTS:

  1. Mpira wa Tz hauwezi kuendelea, katika mill 91 timu inaambulia mill 39!!? Huu ni unyonyaji wa hali ya juu!! Labda niwaulize nyie waandishi ambao kila siku mnasema mnasaidia soka, mmefanya nini kuondoa unyonyaji huu!!?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic