March 14, 2015


Ile ishu ya mshambuliaji wa Simba, Ibrahim Ajibu la kuitumikia klabu hiyo kwenye mechi za ligi kuu wiki iliyopita dhidi ya Prisons na Yanga huku akiwa na kadi nne za njano, linatarajiwa kuchukua sura mpya katika Mkutano Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) utakaofanyika leo na kesho mkoani Morogoro.

TFF ilimruhusu Ajibu kuitumikia Simba katika mechi hizo, ikitumia kanuni mpya za ligi hiyo ambazo zilikuwa bado hazijapata baraka za mkutano mkuu wa shirikisho hilo.

Jambo hilo lilizua utata mkubwa na kusababisha maneno mengi huku uongozi wa Yanga ukidai kuwa utahakikisha unachukua hatua kwa kukata rufaa kupinga uamuzi huo wa TFF.

Baadhi ya wajumbe wa mkutano huo, wamesema watahakikisha suala hilo linajadiliwa ili kukomesha vitendo vya baadhi ya viongozi wa TFF kujichukulia uamuzi mkononi bila ya kufuata taratibu.

“Hakika watendaji wetu wamekuwa wakichemka vibaya sana, hii inasikitisha na inashangaza sana kwani siku zote tunatambua kuwa sheria haiwezi kutumika kama haijapata baraka za rais.


“Hivyohivyo pia katika soka kanuni zetu haziwezi kutumika kama hazijapata baraka za mkutano mkuu, kwa hiyo jambo hilo itabidi tuhakikishe linajadiliwa ili upuuzi uliopo wa watu kujiamulia mambo wao wenyewe uweze kukoma kwa faida ya soka letu,” walisema viongozi hao ambao waliomba kutotajwa majina yao gazetini.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic