Mashabiki Sunderland wamecharuka na kutaka kumvaa kocha wao Gus
Poyet baada ya timu yao kushindiliwa kwa mabao 4-0 na Aston Villa katika mechi ya Ligi Kuu England, leo.
Villa wakiwa ugenini walikuwa wamepata mabao hayo hata kabla ya
mapumziko hali iliyoamsha jazba na polisi na walinzi wa uwanjani kulazimika
kumlinda kocha huyo.
Baadhi ya walinzi walipanda hadi jukwaani kuwapoza mashabiki hao
waliojawa na jazba.
Poyet alikiri kwamba mambo ni mabaya lakini akasisitiza
wataendelea kupambana kujiokoa na balaa la kuteremka daraja.
0 COMMENTS:
Post a Comment