March 14, 2015

 
PRISONSMara baada ya kumtimua kocha wao David Mwamwaja, Prisons imeanza kuonyesha cheche baada ya kuitwanga Stand United kwa mabao 3-0.


Stand iliyoonekana kuwa moto, leo imekiona cha moto katika mechi hiyo ya Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.

Mabao ya Prisons yalipachikwa na Laulian Mpalile, Hamis Maigo na Salum Kamenya aliyehitimisha kazi hiyo katika dakika ya 65..

JKT nayo imeendelea kufanya vizuri baada ya kuichapa Polisi Moro kwa bao 1-0.


Bao la Polisi limefungwa na beki Mohammed Faki katika dakika ya 75.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic