Kocha Mkuu wa Simba, Goran
Kopunovic amesema wako tayari kwa ajili ya Yanga wanayokutana nayo leo kwenye Uwanja wa Taifa, Dar.
Kopunovic amesema kama
mambo yatakwenda kama walivyopanga, basi Simba wategemee burudani na ushindi.
“Sio mechi ya kudharau,
tunajua ina presha kubwa lakini tumezungumza kila kitu na tumeelewana.
“Iwapo mambo yatakwenda
kama tulivyopanga, imani yetu Wanasimba watafurahi. Tunazitaka pointi tatu,
lakini tunajua tunataka Wanasimba wafurahi,” alisema akionyesha kujiamini.
“Yanga ina kikosi bora,
kama utawapa nafasi basi wanakumaliza.
Kikubwa ni kujilinda vema
na kuhakikisha tunatumia nafasi. Kwa kifupi umakini wa hali ya juu unahitajika.”
0 COMMENTS:
Post a Comment